Sports

SAKATA LA KAGERA SUGAR NA SIMBA

Imeandikwa na Admin

Msemaji wa Simba, Haji Manara amewatuhumu baadhi ya viongozi wa TFF kuwa na njama za kuihujumu klabu hiyo.

Manara ameiomba Serikali na Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) kuingilia kati sakata la Simba dhidi ya mchezaji wa timu ya Kagera Sugar, Mohamed Fakhi anayedaiwa kucheza mechi ya Simba ilhari ana kadi tatu za njano kinyume na taratibu na kanuni za TFF.

Manara amemtumia salamu Rais wa TFF kwa kusema kuwa Jamali Malinzi mwisho wake umefika na kudai kuwa haofii kufungiwa na shirikisho hilo kutokana na uamuzi wake wa kusema ukweli kwa ajili ya kutetea klabu hiyo.

Ameyasema hayo leo alipokuwa akiongea na wanahabari.

Related Post