Social

Nyuma ya pazi kifo cha mume wa zari boss lady

Imeandikwa na Admin

Simulizi nzito nyuma ya pazia.
Kwa mujibu wa chanzo cha ndani ya familia ya Ivan iliyopo Muyenga jijini Kampala, kilichokaririwa na mitandao ya kuaminika nchini Uganda, katika siku za mwisho za maisha yake kabla ya kuripotiwa kupatwa na ugonjwa wa shambulio la moyo ambao kitaalam huitwa Coronary Artery Disease (CAD). Ilifahamika kuwa, ugonjwa huo ndiyo uliomsababishia kifo usiku wa kuamkia juzi.

Habari zilieleza kuwa, Ivan alionekana kwa mara ya mwisho kwenye Pati ya Blankets and Wine iliyofanyika huko Kampala, Uganda wiki mbili zilizopita. Ilielezwa kuwa, rais huyo wa Kundi la Rich Gang, mwenye umri wa miaka 39, alionekana aliyedhoofu na asiyekuwa na furaha kama kawaida yake huku akinywa soda na kula samaki, tofauti na alivyozoeleka kuwa ni mtu wa kupiga vinywaji vikali, tena vya bei mbaya. “Nyuma ya hali yake kiafya alionekana dhahiri mwenye matatizo yaliyosababisha hata kula yake kuwa ya kusuasua na kusababisha hali kuwa mbaya zaidi,” kilikaririwa chanzo hicho.
CHANZO CHA UGONJWA
Chanzo hicho kilidai kuwa, chanzo cha Ivan kupatwa na ugonjwa huo ni pale alipotokea Sauzi na kwenda kuangalia moja ya mali zake (mashamba makubwa) zilizopo Kampala na kukuta kuna watu wamebadilisha umiliki bila yeye kujua. Ilisemekana kuwa, kuna wakazi waliotengeneza nyaraka na hati za kumiliki ardhi ya jamaa huyo ambayo ilionesha walikuwa wamiliki wapya ilihali ni mali ya jamaa huyo.
Wakati watu hao wakifanya hivyo, Ivan hakujua kilichokuwa kikiendelea. Ilielezwa kwamba, ishu hiyo ilimsababishia Ivan mshtuko wa moyo na maumivu makali ya kichwa ambayo pia yaliathiri utendaji wake wa kazi wa kila siku.
Mbali na hilo, pia, kuliibuka taarifa za kuuzwa kwa nyumba yake na watu wasiojulikana ambapo alitumia nguvu kubwa kukanusha taarifa hizo na kueleza kuwa kwa utajiri alionao hawezi kuuza nyumba yake ya kifahari iliyopo Munyonyo, Kampala. “Mwishowe, alipoona hali yake kiafya inakuwa mbaya kutokana na mshtuko uliotokana na mambo hayo, Ivan alichukua ndege na kwenda Afrika Kusini kisha kuripoti mwenyewe katika Hospitali ya Steve Biko Academy iliyopo Pretoria. “Vipimo vilionesha kuwa alipatwa na mshtuko wa moyo ambao ulisababishwa na kuganda kwa damu kwenye mishipa,” RIP IVAN

Related Post