Politics

Lowassa apatiwa msaada wa kisheria

Imeandikwa na Admin

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (#CHADEMA) kimetoa maelekezo kwa Kurugenzi ya katiba na sheria kuhakikisha wanampatia msaada wa kisheria Waziri mkuu mstaafu, Mh. #EdwardLowassa aliyepata wito wa kufika makao makuu ya polisi leo saa nne asubuhi.

Kupitia taarifa iliyotolewa na Idara ya mawasiliano CHADEMA, Mkuu wa idara ya habari Tumain Makene amesema Mh. Lowassa amepata wito kutoka kwa Mkurugenzi wa makosa ya jinai (DCI) ambaye amemtaka afike leo saa nne asubuhi bila kupewa maelezo wala ufafanuzi juu ya nini kitajiri katika mahojiano.

 

Related Post