Politics

Makonda: Marufuku watendaji wa Dar es Salaam kutoka nje ya mkoa

Imeandikwa na Admin

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amepiga marufuku watendaji wa Mkoa huo kutoka nje ya mkoa bila kutoa taarifa kwa mkuu wa Mkoa Makonda amepiga marufuku hiyo leo wakati wa kongamano la tathimini ya hali ya miundombinu ya barabara za mkoa huo unaoendelea katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere.

Kauli hiyo ya Makonda imekuja baada kukosekana kwa watendaji ambao walitakiwa kuhudhuria kongamano hilo kwa madai kuwa wako nje ya mkoa kikazi huku waliobakia wakishindwa kueleza kuwa wapo kwaajili ya kazi gani.

” Kuanzia sasa hakuna mtumishi wa Mkoa huh kutoka nje bila kutoa taarifa hata kama ni kazi ya Wizara gani lazima mtoe taarifa, kumekuwa na tabia ya watu kujitengenezea tu safari ambazo hazijulikani wakati hata rais wetu alishazikataza,” alisema Makonda

Related Post