Entertainment

Ruby amtolea Povu Nandy

Imeandikwa na Admin

Mwanamuziki Ruby aliyefanya poa na ngoma ya ‘Na Yule’ amewataka mashabiki zake wasijichanganye kwa kumfananisha na Mwanamuziki ‘Nandy’ anayetamba sasa na ngoma ‘Wasikudanganye’ kwa kuwa kamwe msanii huyo hawezi kufanya vitu ambavyo yeye anafanya.

RUBY

RUBY

Akizungumza na EATV Website, Ruby ambaye amekuwa kimya kwa kipindi kirefu kidogo amesema kuwa uwezo alionao wa kufanya muziki ni mkubwa na ana uwezo wa kufanya zaidi ya alivyowahi kuonyesha hapo mwanzoni.

“Nandy ni msanii wa kike ambaye ni chipukizi amenikuta kwenye game mimi ni msanii mkubwa sana kwake kwa. Vitu anavyovifanya mimi ninauwezo wa kufanya zaidi yake. Watu wakisema kwamba ameniacha mbali kimuziki watakuwa wanakosea kwani mimi ni wa kwanza kuliona jua kabla yake,” Ruby amefunguka

Nandy

Nandy

Pamoja na kufananishwa aina ya uimbaji wao Ruby ameongeza kwamba ” Nandy nimeshawahi kukutana naye mara chache na niseme hawezi kuimba kama mimi. Ila mimi Ruby nina uwezo wa kuimba kama yeye na labda siku moja ninaweza kuimba kama anavyofanya Nandy ili watu wasitufananishe tena”.

Akizungumzia kutoa nyimbo kwa mfululizo ili kwendana na kasi aliyonayo Nandy mwanadada huyo ambaye amegoma kutaja uongozi wake wa sasa amesema katu hawezi kutoa nyimbo mfululizo kwani kila mtu ana soko lake.

“Siwezi kutoa nyimbo mfululizo lakini nitoe ahadi sitaweza kukaa kimya tena .

Related Post