Entertainment

Gigy Money Akataa Mahari Ya Milioni 5

Imeandikwa na Admin

MUUZA nyago kwenye video ambaye pia ni msanii wa Bongo Fleva, Zawadi ( Gift ) Stanford ‘#GigyMoney’ amejikuta akipishana na bahati baada ya kugomea mahari ya shilingi milioni 5 kutoka kwa mwanaume aliyetaka kumuoa.

Akizungumza na Star Mix, #Gigy anayebamba na Wimbo wa #Papa alisema, siyo kama hapendi kuolewa lakini anachoangalia ni thamani yake kwanza ambayo kama ni kutolewa mahari basi iwe zaidi ya milioni 5.

“Namshukuru Mungubahati ya kuolewa ninayo, lakini watu wanashindwa kutekeleza mahari yangu ninayotaka na sioni haja ya kukiuka kigezo changu sababu kama ridhiki ipo ipo tu.

“Kuna Jamaa alileta posa, lakini alivyopewa hilo sharti la milioni 10 jasho likamtoka, akalilia milioni 5 nikagoma, huo ndiyo msimamo ila uamuzi wa mwisho ni Muumba siwezi jua huenda kapuku akaniopoa huko mbeleni,”

Related Post