Politics

Halima Mdee aitwa na Jeshi la Polisi Tanzania

Imeandikwa na Admin

Jeshi la Polisi nchini limewataka watu mbalimbali akiwemo Mbunge #HalimaMdee, walioripoti kwenye mitandao ya kijamii na kusambaza picha ya askari wake akihusishwa na tukio la #TunduLissu kuripoti kwa DCI kwa ajili ya mahojiano zaidi.

Taarifa hiyo imetolewa leo na msemaji wa Jeshi la Polisi nchini ACP Barnabas David kwenye mkutano wake na waandishi wa habari, na kuwataka watu hao akiwemo mbunge huyo wa Kawe kwa tiketi ya #CHADEMA kujisalimisha wenyewe kwa kutoa taarifa za uongo.

ACP David ameendelea kwa kusema kwamba jeshi la polisi kitengo cha upelelezi wa makosa ya mtandaoni kinaendelea na uchunguzi, kuwabaini wote waliohusika na kusambaza kwa taarifa hizo za uongo ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

Related Post