Politics

JPM afuta umiliki wa mashamba ya vigogo

Imeandikwa na Admin

Rais #JohnMagufuli amefuta umiliki wa mashamba mawili makubwa katika eneo la Kigamboni na kuyarudisha serikalini likiwemo la Amadol lenye ekari 5,400 na lililokuwa likimilikiwa na mfanyabiashara Yusuf Manji lenye ekari 715.

PIA

Rais wa Jamhuri wa Muungano wa #Tanzania John Pombe Magufuli amevunja Mamlaka ya uendelezaji wa Mji wa Kigamboni (KDA) kuanzia leo Septemba 13, 2017

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Hashim Mgandilwa amethibitisha hilo na kusema kuwa Rais Magufuli ni msikivu kwani amesikia kilio cha watu wa Kigamboni na kuamua kuivunja mamlaka hiyo ya Uendelezaji wa Mji wa #Kigamboni (KDA). “Usikivu ni sehemu ya utatuzi hatimaye Rais wa Jamhuli ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli aridhia uvunjwaji wa Mamlaka ya uendelezaji wa mji wa Kigamboni (KDA). Akizungumza Waziri wa Ardhi Mhe. Lukuvi leo katika ukumbi wa chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere amesema “Mhe. Rais ameniagiza niwaalifu kuwa leo amevunja rasmi KDA, Ahsante Mhe. Rais kwa kutusikiliza” alisema Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mgandilwa

Mwezi Juni, mwaka huu #Mbunge wa Kigamboni, Dk Faustine Ndugulile aliiomba serikali kukabidhi majukumu yote, yaliyokuwa yakifanywa na KDA kwa Halmashauri ya Manispaa hiyo ili kuyatekeleza na kuendeleza mji mpya wa Kigamboni.

Related Post