Business Social

Kiwanda cha nyaya za umeme chawaka moto

Imeandikwa na Admin

Kiwanda chote cha Multi Cable Limited kilichopo eneo la Kijereshi kata ya Igoma jijini Mwanza ,kimeteketea kwa moto leo.

Kiwanda hicho kimeanza kuwaka saa nne mchana kutokana hukuchanzo kikibainika ni hitilafu ya nguvu za umeme.

Kiwanda hicho cha Multi Cable Limited kinajihusisha na utengenezaji wa nyaya za umeme na bomba za kupitisha nyaya hizo.

Mmoja kati ya wafanyakazi wa kiwanda hicho, anasema wao walishtukia moshi ukiwa unatokea kwenye ‘store’ wakagundua kwamba ni nyaya zimegusana kwenye paa na kusababisha moto huo.

Related Post