Entertainment Social

Madame Wema amsapoti Zari Hamisa Mobetto. Huddah Monroe amrushia kijembe Zari.

Imeandikwa na Admin

Madame #Wemasepetu amsapoti #Zarithebosslady na kuwatelekeza wengi wa #TeamWema wanaomsapoti #HamisaMobetto. #HuddahMonroe amrushia kijembe #Zari.

#WemaSepetu amesema Kama mwanamke ukiwa nafasi ya Zari lazima uumie “Najua( Zari) anaweza kusema maneno ya ovyo juu yangu, lakini najua hali anayopitia kama mwanamke, nadhani sasa ni wakati muafaka kwake(Diamond) kuweza kumvisha pete, mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni,” amesema Wema ambaye uhusiano wake na Diamond uliwahi Kuwa habari ya mjini kila kona ya nchi Kabla ya kumuacha Diamond ambapo baadaye walikutana na Zari

Kwa upande mwingine Huddah Monroe ambaye aliwahi kudaiwa kutoka na Diamond kipindi cha nyuma amemrushia Dongo Zari kwa kusema mwanaume Ni wako akiwa kwako akitoka nje si wako .

Huddah na Zari walikuwa marafiki wakubwa kipindi cha nyuma lakini Zari alipoanza Kuwa karibu na Vera Sidika anayetajwa Kuwa hasimu mkubwa wa Huddah ndio hapo Huddah na Zari urafiki wao ukaanza kuchacha na kuharibika kabisa .

Related Post