Entertainment

Aliyekuwa mume wa Uwoya achachawa na ndoa ya Dogo Janja na Irene Uwoya

Imeandikwa na Admin

Siku chache baada ya kusambaa kwa picha za harusi za aliyekuwa mke wake ambaye ni #Queen wa Bongo Muvi, #IreneUwoya, kuonekana amefunga ndoa na mwanamuziki nguli wa Bongo Fleva, #DogoJanja, msakata kabumbu #Hamad #Ndikumana ‘Kataut’, ameonekana kuumizwa na ndoa hiyo.

Licha ya kuwa kwa sasa ana mpenzi mwingine, lakini kutokana na maneno yake mitandaoni mashabiki wanadai anaumwa homa ya wivu.

Ndikumana ambaye hasira za kumuanika mpenzi wake mpya zilianza baada ya kumuona mzazi mwenziye kafunga ndoa na Janja, ambapo mashabiki walitarajia baada ya kila mmoja kupata pumziko lake hakutakuwa na maneno tena. Lakini imekuwa tofauti kwani mwanasoka huyo ameendelea kuposti picha kupitia mtandao wake wa Instagram na kuiambatanisha na ujumbe unaoelezea jinsi ambavyo mama yake anamhurumia kwa jinsi alivyokuwa amepotea njia kumuoa Uwoya, na sasa amepata jiko jipya anampongeza.

Irene na Ndikumana walifunga ndoa mwaka 2009 na kufanikiwa kupata mtoto mmoja wa kiume waliyempa jina la #Krish, lakini ndoa yao haikudumu kwa muda mrefu wakatengana, ambapo hivi karibuni kumeenea taarifa kwamba Diva huyo amefunga ndoa na Dogo Janja, kutokana na picha zao za harusi zinazosambaa mitandaoni, lakini Uwoya mwenyewe amekanusha ishu hiyo na kusema hajafunga ndoa na Janja, badala yake ni Muvi inayotarajiwa kutoka hivi karibuni.

Related Post