Entertainment Social

Baba Kanumba ailalamikia Mahakama kuwa imempa LULU hukumu ndogo kama ameua kuku

Imeandikwa na Admin

Baba Kanumba amelalamika kuwa mahakama imempa #ElizabethMichael #Lulu hukumu ndogo Kama Kaua kuku


“Kwa upande wangu hukumu hii kwa nini imekuwa ndogo sana? Na haijanifurahisha sana hata kama mtu aliua kwa kutokukusudia lakini mahakama imetoa kifungo cha miaka miwili, kama mtu kaua kuku. Nilitegemea mahakama ingetoa kifungo kuanzia miaka mitano, sita au saba na kuendelea.” Amesema Baba Kanumba akizungumza na GPL ambapo pia siku za nyuma yeye na Mama #Kanumba waliripotiwa kuingia katika mkwaruzano sababu ya mali alizoacha Kanumba

Anyway, nini maoni yako, unadhani Lulu akimaliza adhabu alopewa na mahakama wazazi wa Kanumba hawatakuwa na tatizo nae tena sababu mama Kanumba tayari ameipongeza na kuishukuru mahakama kwa adhabu iliyompa Lulu?

Related Post