Entertainment

Baraka the prince afungukia kufeli kwake

Imeandikwa na Admin

Msanii #BarakaThePrince amemlaumu meneja wake wa zamani chini ya #RockStar 4000 Seven Mosha pamoja na mpiga picha maarufu #MxCarter, kuwa ndio wanaohusika na kufelisha kazi yake mpya #YouTube.
#Baraka ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye eNewz ya East Africa Television, na kusema kwamba watu hao wawili ndio walikuwa na ‘access’ ya acount yake ya YouTube, hivyo wao ndio watakuwa wahusika.
Baraka ameendelea kwa kusema kwamba mara ya kwanza walimfanyia hivyo kwenye acount yake ya zamani ambayo ilikuwa inasimamiwa na RockStar 400, views zilikuwa zinapungua badala ya kuongezeka huku wengine waklimlalamikia kuwa hawaioni YouTube, hivyo aliamua kuifuta na kufungua mpya, na hata hivyo waliendelea kufanya hivyo kwa acount hiyo mpya.

Related Post