Entertainment Social

Hamisa Mobetto adaiwa kumfanyia ukatili mwane aliyezaa na diamond

Imeandikwa na Admin

SIKU chache baada ya kutoswa malezi ya mwanaye, #AbdulNasibu ‘#PrinceAbdul’ ambapo alimfungulia kesi mahakamani ya madai ya malezi mzazi mwenziye ambaye ni msanii wa Bongo Fleva, lakini Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar, upande wa Watoto ukatupilia mbali shitaka hilo, mwanamitindo maarufu Bongo, #HamisaMobetto anadaiwa kumfanyia ukatili mwanaye huyo.

TUJIUNGE NA CHANZO

Chanzo makini kilicho karibu na familia ya #Mobeto kililimwagia ubuyu kwetubongo kuwa, mrembo huyo, licha ya kuwa mtoto wake bado mdogo ana umri wa miezi minne, amekuwa akimtelekezea mama’ke mzazi, Shufaa Lutigunga na kusafiri mara kwa mara nje ya nchi. “Yaani kwa kweli inatushangaza sana, kweli mtoto ana umri wa miezi minne, unaanzaje kumuacha na kwenda mbali kiasi hicho? “Mara utasikia leo yupo Nairobi, mara utasikia yupo Dubai sasa hapo unategemea nini?,” kilimwaga ubuyu chanzo hicho.

CHANZO CHAZIDI KUTIRIRIKA

Chanzo hicho makini kiliendelea kutiririka kuwa, Mobeto tangu ajifungue, amekuwa akisafiri mno na kumwacha mtoto, jambo ambalo linawapa maswali watu wengi kwamba, ina maana hamnyonyeshi hivyo
anaweza kumfanya mtoto adumae kwani maziwa ya mama ni muhimu kwa mtoto mchanga katika miezi sita ya kwanza. “Kila mtu anafahamu umuhimu wa maziwa ya mama kwa mtoto mchanga hususan katika kipindi cha miezi sita ya awali, tunatilia shaka sana anaweza hata kumbemenda mtoto maana hatujui kule anaenda kukutana na wanaume tofauti, akishiriki nao je?” Kilihoji chanzo hicho.

MOBETO ANASEMAJE?

Ili kuujua ukweli wa habari hizo, kwetubongo kama ilivyo desturi yake ya kupata mzani (balance), lilimtafuta Mobeto ambapo mazungumzo yalikuwa hivi;
Kwetubongo: Habari yako, ninaongea na Mobeto?

Mobeto: Ndiyo, nani mwenzangu?
Kwetubongo: Unaongea na Gazeti la Kwetubongo hapa.
Mobeto: Okey, sema…
Kwetubongo: Kuna habari kwamba umekuwa ukimtelekezea mama yako mtoto na kusafiri mara kwa mara na juzi tu ulikuwa Dubai ulikokwenda kujirusha na baba mtoto wako, msanii wa Bongo Fleva, unazungumziaje?
Mobeto: No coment…. (akakata simu).

Related Post