Entertainment

Hivi ndivyo dkt shika anavyokula bata la uzeeni

Imeandikwa na Admin

Mmoja wa mameneja wa Dk. Shika ambaye hakupenda jina lake lichorwe gazetini, amethibitisha kwamba tangu aanze kumsimamia mzee huyo, amekuwa akipata michongo kibao kila siku.

TUMSIKILIZE MENEJA
“Daah kwa kweli ni michongo mingi sana ya hela. Yaani simu kila wakati inaita. Watu wanamhitaji kweli Dk. Shika, kwa siku napokea si chini ya simu hamsini mpaka sitini,” alisema meneja huyo.

AZICHUJA SIMU
Meneja huyo alisema, baada ya kuona simu hizo zimekuwa nyingi, wamelazimika kuwa wanazichuja kulingana na namna mtu anavyojieleza kwani wengi wao wamekuwa wakitoa michongo ya fedha ndogo. “Unakuta mwingine anakuambia eti anataka kupiga naye picha akupe elfu tano, elfu kumi hizo kwa kweli tumelazimika kuziweka pembeni si kwamba ni ndogo lakini kwa kweli tukiruhusu hizo hatutaweza kuwahudumia wote.
WANAANZIA MILIONI
“Na badala yake tunapokea dili zile zinazoanzia milioni na kuendelea tena kwa kuangalia watu ambao wapo serious,” alisema.
DILI ALIZOWEKA KIBINDONI
Meneja huyo alisema si vyema kuzinadi dili zote na kiasi alicho nacho kwa sasa lakini akasema itoshe tu kusema kwa sasa dili za kuwaingizia mamilioni ya kutosha zimeingia na zinaendelea kuingia. “Tunamshukuru Mungu kwa kweli. Amefungua milango yake tunaingiza dili za fedha. Kuna wengine wanataka tu ‘appearance’ ya muda mfupi na wengine wanataka mkataba wa muda mrefu. “Mfano, Vodacom wao walituita tu ofisini kwao, tukawa na appearance pale na wafanyakazi wao, tukala nao chakula pamoja wakatulipa tukaondoka zetu.

ROMA NA STAMINA
“Kuna wasanii wengi wameshatufuata, wengine tupo nao kwenye mazungumzo lakini ambao tayari tumeshafanya nao kazi na imetoka ni Roma na Stamina katika wimbo wao wa Kiba 100,” alisema meneja huyo.

MATANGAZO YA JUISI
Sambamba na madili hayo, meneja huyo pia alisema kuna dili za bidhaa mbalimbali za juisi ambazo tayari zimeshawalipa na wameshatangaza bidhaa zao.

WAREMBO WAMGOMBEA
Kama hiyo haitoshi, meneja huyo alisema mbali na michongo hiyo ya fedha, warembo kibao wamekuwa wakimgombea kila wanapokatiza katika hoteli mbalimbali za kifahari wanazofika wakitaka kupiga naye picha. “Unajua dokta kwa sasa kutokana na jina lake hawezi kulala sehemu moja. Analala hoteli mbalimbali za kifahari.

Related Post