Entertainment Social

Mahakama Kuu ya Tanzania Leo imemuhukumu miaka jela 2 Elizabeth Michael ‘Lulu’

Imeandikwa na Admin

Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano wa #Tanzania, leo Novemba 13 imemuhukumu miaka jela 2 #ElizabethMichael ‘#Lulu’ kwa kosa la kumuua msanii mwenzake #StevenKanumba bila kukusudia.

Elizabeth Michael (Lulu) anahukumiwa kwa kumuaa aliyekuwa mpenzi wake Steven Charles Kanumba ambaye pia ni muigizaji mwenzake, mnamo April 7, 2012, wakati tukio hili linatokea Lulu alikuwa na miaka 17 na sasa anamiaka 22.

Kesi hiyo ambayo ilianza kusikilizwa tena Oktoba 19 mwaka huu, ilianza kwa kusikiliza ushahidi wa pande zote mbili za mashtaka na mshtakiwa, na kisha kusikiliza maoni ya wazee wa baraza la mahakama na hatimaye mahakama kumkuta #Elizabeth na hatia ya kuua bila kukusudia.

Elizabeth Michael anatuhumiwa kumuua bila kukusudia aliyekuwa mpenzi wake na muigizaji mwenzake, Steven Charles Kanumba, mnamo April 7, 2014.

Related Post