Entertainment

Mama Kanumba alipoulizwa Kama amepanga kumtembelea Lulu

Imeandikwa na Admin

Mama #Kanumba alipoulizwa Kama amepanga kumtembelea #Lulu gerezani siku za usoni baada ya kuhukumiwa jela amejibu kuwa hajui hadi azungumze kwanza na Mungu wake. “Sijui inabidi nimuulize Mungu wangu, inabidi nikae nimuulize Mungu wangu” Amesema Kupitia kipindi cha #Shilawadu

Pia amedai Lulu kumuita kubwa jinga, ameongeza kuwa Lulu alivyotoka segerea alijifanya mtu mwema kwake kumbe sivyo ili Watanzania wasahau mambo yake yamuendee vizuri. Mama Kanumba amesema hajaridhishwa na hukumu alopewa Lulu miaka 2 yeye angefurahi Kama angefungwa miaka 5 hadi 10 Kama alivyosema baba Kanumba kuwa hukumu alopewa ndogo Sana Kama Kaua kuku. .

Kwa upande Mwingine Mama Kanumba amesema Wema Sepetu ndie mwanamke pekee aliyekuwa na sifa za kuolewa na mwanae, amesema anachompendea Wema ni kumkubali kuwa Kanumba ndie kamuingiza Kwenye filamu.

Wema na Kanumba waliwahi kuwa wapenzi, mwaka 2009 Wema kwa hasira alivunja kioo cha gari la Kanumba chenye thamani ya sh.million 1 na kupelekwa mahakamani lakini baadaye Kanumba aliifuta kesi hiyo .

 

Related Post