Politics

RAIS DKT MAGUFULI AMPONGEZA RC MAKONDA

Imeandikwa na Admin

Rais Dkt John Pombe Magufuli leo asubuhi akiwashukuru na kuwaaga madaktari wa meli ya kijeshi ya China, ambayo imetibu wagonjwa zaidi ya 5000 kwa wiki moja, amemshukuru pia Mkuu wa mkoa wa DSM, Paul #Makonda kwa kuratibu vizuri zoezi hilo, akisema:

“Hata kama kuna watu hawampendi,lakini yeye anawapenda sana na anahangaika sana na Wananchi wa mkoa wake.” “Nilimuona wakati fulani akihangaika kuwatafutia miguu walemavu wa ajili ya watu wake,nilijiuliza vipi huko kwingine hakuna walemavu? ”

“Nilipomuona wakati fulani akienda kwenye kiwanda cha magodoro Dodoma kuomba magodoro 1000 kwa ajili ya wagongwa wa mkoa wake,nilijiuliza hivi kule Dodoma hawapo wagonjwa?”

“Nilipomuona akienda kutengeneza magari ya polisi kule Moshi, nilijiuliza hivi kule Moshi magari yote ya polisi ni mazima?” “Ninawashauri viongozi wote serikalini waige mfano huo.”

Related Post