Sports

Samatta nje wiki sita, kuikosa Benin

Imeandikwa na Admin

NAHODHA wa timu ya soka ya Taifa ya #Tanzania ‘#TaifaStars’, #MbwanaSamatta, atakuwa nje ya uwanja kwa kipicha cha wiki sita baada ya kuumia goti.

#Samatta aliumia goti Jumamosi iliyopita kwenye mchezo wa timu yake dhidi ya Lokeren wa Ligi Daraja la Kwanza A nchini Ubelgiji.

Baada ya kufanyiwa uchunguzi, Samatta amegundulika kupasuka mishipa midogo ya goti lake la mguu wa kulia, hivyo anahitaji kufanyiwa upasuaji ili kutibu jeraha hilo.

“Kuchanika kwa mishipa hii inaweza ikanisababishia kukaa nje ya uwanja kwa wiki sita au na zaidi ili kuweza kupona kabisa,” alisema Samatta.

Kutokana na hali hiyo, Samatta ataukosa mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Benin utakaochezwa nchini humo Jumamosi wiki hii.

Alipotafutwa kocha Taifa Stars, Salum Mayanga, kuelezea kukosekana kwa nyota huyo, hakuwa tayari kuzungumza kwa kuwa alikuwa akisimamia mazoezi ya timu hiyo jana jioni.

Hata hivyo, Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (#TFF), Alfred Lucas, aliliambia Nipashe kuwa bado hawajapokea taarifa hiyo kutoka klabu ya KRC Genk.

“Taarifa ambazo tunazo ni kuwa Samatta aliumia goti kwenye mchezo wao uliopita, lakini alitarajiwa kufanyiwa uchunguzi kujua ukubwa wa tatizo lake, mawasiliano yetu tuliambiwa tutapata uthibitisho kama Samatta ataungana na timu kesho au keshokutwa,” alisema Lucas.

Alisema pindi watakapopata taarifa rasmi watatoa maelezo kupitia kwa kocha Mayanga.

Related Post