Politics

TAARIFA-CHADEMA KANDA YA KASKAZINI 12.11. 2017

Imeandikwa na Admin

Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya #CHADEMA Taifa Mhe.#EdwardNgoyaiLowassa, Jana novemba 12 amezindua Kampeni ya udiwani katika kata ya Moita Jimbo la #Monduli kwa kufanya Mkutano mkubwa wa hadhara uliohudhuriwa na maelfu kwa maelfu ya wananchi wa kata hiyo, Mhe.#Lowassa alimnadi mgombea udiwani wa kata hiyo kwa tiketi ya CHADEMA Ndugu.Lobulu Lerango.

Akizungumza katika Mkutano huo Mhe.Lowassa alisema watu wa Moita hawajawai kushindwa hivyo aliwataka wafanye kazi kubwa ya kulinda kura siku ya 26.11.2017.

Pia mkutano huo ulihutubiwa na Katibu wa CHADEMA Wilaya ya Monduli Mhe.Hussein Ole kuney, #Mbunge wa Jimbo la Monduli Mhe.Julias Kalanga, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli Mhe.Isack Joseph pamoja na Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Arusha ambao ni Mhe.George Nditika na Mhe. Ally Bananga.

Kampeni za uchaguzi wa Marudio ya udiwani zinaendelea sehemu mbali mbali Kanda ya Kaskazini. *Imetolewa na;*
*Mozec Joseph* *Afisa-Habari CHADEMA Kanda ya Kaskazini.*

Related Post