Politics

CHADEMA kimekanusha taarifa kuhusu Mnyika

Imeandikwa na Admin

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (#CHADEMA) kimekanusha taarifa zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii kuwa Mbunge wa Kibamba, John Mnyika amejivua uanachama wa chama hicho.

Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana. Kuhusu masuala mbali mbali yanayohutu tume ya Katiba. Picha na Emmanuel Herman

Disemba 3 kuanzia majira ya alasiri zilianza kusambaa taarifa zinazodai kuwa mbunge huyo amekihama chama hicho na kujiunga Chama cha Mapinduzi (#CCM). Taarifa hiyo ilikuja ambapo kwa siku za hivi karibuni tumeshuhudia wimbi kubwa la watu wakihama kutokana chama kimoja kwenda kingine, kwa madai ya kutoridhishwa na mwenendo wa chama walichotoka.

Kupitia kurasa zao zi mitandao ya kijamii, CHADEMA wamewataka wananchama wao na wananchi kwa ujumla kupuuza madai hayo na kwamba waliokosa majibu kuhusu hali ya watanzania, ndio wanaosambaza taarifa hizo za uongo.

“Kuna taarifa zinasambazwa mitandaoni ya kuwa Mhe. John Mnyika, Mbunge wa Kibamba amejivua uanachama wa CHADEMA. Taarifa hizo ni za uongo na hazina ukweli wowote, ni za kupuuzwa, wanaozisambaza ni wale walioishiwa hoja na majibu juu ya hali ya maisha ya Watanzania.”
.

Related Post