Politics

Mbunge wa CUF ahamia CCM

Imeandikwa na Admin

Aliyekuwa #Mbunge wa #Kinondoni kupitia #ChamaChaWananchi (#CUF), #MaulidMtulia amekabidhiwa rasmi kadi ya Chama Cha Mapinduzi (#CCM) mapema leo katika ofisi za chama hicho.

Mwanasiasa huyo alitangaza kijivua uanachama cha CUF siku ya jana, ambapo alisema kuwa ahadi zote alizoziahidi zinatekelezwa na Rais Magufuli hivyo haoni haja ya kuwa mpinzani. Hata hivyo Chama cha wananchi (CUF) upande wa Profesa Lipumba, kimesema aliyekuwa mbunge wa Kinondoni kupitia chama hicho Maulid Mtulia alikuwa anakihujumu chama kwa muda mrefu

Afisa habari wa chama hicho, Abdul Kambaya amesema Mtulia alishawahi kujitoa kugombea udiwani dakika za mwisho mwaka 2005.

Pia aliwahi kujaza vibaya fomu ya kugombea ubunge mwaka 2015 na kusababisha #NEC kumuondoa

Related Post