Politics

Mhe. Lissu atumiwa kikosi cha wapelelezi kwa mahojiano Nairobi

Imeandikwa na Admin

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, #IGP #Simon #Sirro, amesema timu yake ya wapelelezi imetumwa kwenda jijini Nairobi, nchini Kenya kufanya mahojiano na Mhe. #Tundu #Lissu pamoja na dereva wake.. Tangu Mhe. #Lissu ashambuliwe kwa risasi na watu wasiojulikana mwezi Septemba 7, mwaka huu mjini Dodoma, Polisi ilikuwa bado haijafanya mahojiano naye.

IGP Sirro amesema wametuma wapelelezi Nairobi baada ya kusikia Lissu amekubali kuhojiwa juu ya tukio hilo na matarajio yao pia ni kumpata dereva na mlinzi wake. “Tumetuma watu wetu kwenda kuchukua maelezo yake (Lissu)..Mwanzo tuliomba kwenda lakini chama (#Chadema) walikataa. Juzi tumesikia wamesema wapo tayari…Tumetuma vijana wetu wawili kwenda Nairobi kuchukua maelezo yake.”amesema IGP Sirro.

IGP Sirro amesema lengo kubwa la mahojiano ni kujua mazingira ya shambulio yalikuwaje na kwamba ikiwezekana wampate dereva na msaidizi huyo wa Lissu ili kurahisisha upepelezi wa tukio lenyewe. “Upelelezi unaingia vitu vingi sana (sasa) kutompata dereva na mlinzi wake Lissu inashindwa kutupa picha kamili ya tukio,” alibainisha IGP Sirro huku akiwataka Watanzania kuwa na imani na jeshi la polisi katika kufuatilia tukio hilo. “Niwaambie Watanzania watuamini, hatuko kwa ajili ya kuona hatumtendei mtu haki, tupo kwa ajili ya kutenda haki.”amesema IGP Sirro.

Related Post