Entertainment

WEMA Atahadharishwa na SHAMSA

Imeandikwa na Admin

KUFUATIA kuhama chama kutoka Chadema kwenda CCM kwa mwanadada kutoka kiwanda cha filamu Bongo, Wema Sepetu, msanii mwenzake, Shamsa Ford ameibuka na kumtahadharisha pamoja na wasanii wote kwa jumla.

Akipiga stori nasi, Shamsa alisema wao siyo wanasiasa hivyo suala la Wema la kwenda na kurudi kwenye vyama vya siasa inawezekana anapata faida lakini cha muhimu asisahau kazi yake.

“Siwezi kuzungumzia sana suala la Wema kuhama vyama maana ni lake binafsi na huenda lina faida kwake, nawasihi tu wenzangu wasisahau kazi yao ya sanaa iliyowatambulisha kwa jamii,” alisema Shamsa.

Related Post