Entertainment

BARAKA THE PRINCE AFUNGUKA KUVURUNDA 2017

Imeandikwa na Admin

Msanii wa muziki, #BarakaThePrince amefunguka kueleza kilichomfanya ashindwe kufanya vizuri kimuziki mwaka 2017.

Muimbaji huyo ambaye mwaka 2017 aliachana na label ya Rock Star4000 na kuanzisha label yake, Bana Music, amedai sababu iliyomfanya ashindwe kufanya vizuri ni kukataa baadhi ya show ambazo alikuwa anapewa na mapromota. “Mi nimiongoni mwa wasanii ambao nabagua sana show, mpaka nikifanya show mpaka promota afike bando ambalo nahitaji, na ninafaya hivyo ili kulinda brand yangu ambayo tayari nimeshaitengeneza,” Baraka alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio.

Aliongeza,”Na kama nimeyumba kimaisha nayumba kweli kwa sababu maisha ndivyo yalivyo, kuna kupanda na kushuka, mpaka mataifa mkubwa wanayumba kiuchumi mimi ni nani, sio kitu kibaya, kinaweza kumtokea mtu yeyote”, Hivi karibuni kumekuwa na malalamiko kutoka kwa maashabiki kuwa msanii huyo sio tu amefulia, bali hata uwezo wake kwenye kazi umeshuka, na kushauri kama inawezekana awe anaandikiwa kazi zake.

Related Post