Entertainment

Mchumba wa Wolper afunguka Mengi

Imeandikwa na Admin

Anayedaiwa kuwa ni mchumba wa muigizaji #Jaqueline #Wolper , Engine amesema kwamba yeye ana mahusiano ya muda mrefu na muigizaji huyo na wala siyo kwamba amekurupuka kama watu wanavyofikiria.

#Engine amelazimika kufunguka hayo baada ya habari mitandaoni kusambaa kwamba wiki iliyopita alikwenda kumvalisha pete ya uchumba huko kwa bibi yake Moshi.

Engine amesema kwamba japokuwa hawezi kusema ni muda gani amekaa kwenye mahusiano na mrembo huyo lakini anachoamini ana muda mrefu na wameshachunguzana na kwamba wameona sasa ni muda muafaka wa wao kuwa baba na mama.

Engine amesema kwamba hayo mambo mengine yanayoendelea mitandaoni kuhusu mahusiano yao pamoja na aliyekuwa mpenzi wa Wolper wa zamani, Mwanamitindo Brown yeye hana muda nayo kwa kuwa yupo bize na kazi zake na anategemea muigizaji huyo atakuwa mama wa familia yake.

Aidha mpenzi huyo wa Wolper ambaye pia ni mwanamuziki Chipukizi amesema kwamba mahusiano yake yasifananishwe na wale wanaume wanaotafuta jina kupitia mrembo huyo ndiyo maana hata mambo yao hawajawahi kuyaanika mitandaoni kwa kuhofia maneno ya watu pamoja na ndele.

Related Post