Politics

Meya wa Ubungo na Temeke wapigana Live

Imeandikwa na Admin

Jana mchana hiyo kwenye uchaguzi wa Naibu Meya ndani ya ukumbi wa Karimjee,jijini Dar. Videoni ni marumbano na kurushiana maneno baada ya meya boniface na Chaurembo kukunjana… ‘Ilikuwa mshike mshike….

Meya wa Ubungo Boniphace Jacob na Meya wa Temeke Abdallah Chaurembo wakizichapa ‘kavu kavu’ mapema jana ndani ya ukumbi wa Karimjee wakati wa uchaguzi wa Naibu Meya . ——. ——- ——- ——
Kutoka hapa Karimjee, DSM. UKAWA imeshinda nafasi ya Unaibu Meya wa Jiji la DSM baada ya Diwani wa Chama Cha Wananchi CUF (#CUF Taasisi) Mhe. Kafana (Dk. Kimimbi) kupata kura 12 dhidi ya kura 10 za Bi. Mariam (Mgombea wa CCM ambaye pia ni diwani wa CCM). Jumla ya wapiga kura wote walikuwa ni 22, #CCM ikiwa na wapiga kura 11 na UKAWA (Chadema na CUF) ikiwa na kura 11.
Ilitegemewa kwamba kura zingefungana 11 kwa 11 na kwa mujibu wa kanuni za Jiji, SARE hiyo ingelikuwa na maana kuwa Naibu Meya kutoka CUF angeongoza jiji kwa miezi 6 na kumpisha wa CCM aongoze miezi 6.

Mussa Kafana (Aliyebebwa) ameshinda uchaguzi wa Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam na hapa ni alipokuwa akipelekwa kupiga kura katika uchaguzi huo uliogubikwa na vurugu na Kukunjana.

Related Post