Business Social

Mke bilionea Msuya kusubiri Januari 22

Imeandikwa na Admin

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam imepiga kalenda kesi ya mauaji inayomkabili mke wa marehemu bilionea Erasto Msuya, Miriam Mrita, na mwenzake hivyo kuendelea kusota mahabusu.

Mke wa marehemu bilionea Erasto Msuya, Miriam Mrita

Wawili hao wanakabiliwa na kesi ya mauaji ya dada wa bilionea huyo, Aneth Maurya, ambayo itaendelea Januari 22.

Kesi hiyo ilitajwa jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Willard Mashauri, baada ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba aliyepangiwa kusikiliza usikilizwaji wa awali kuwa na udhuru.

Wakili wa Serikali, Sekiwanga Nalindwa alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika, hivyo aliomba tarehe nyingine ya kutajwa.

Hakimu Mashauri alisema kesi hiyo itatajwa tena Januari 22 na washtakiwa wataendelea kukaa mahabusu.

Mbali ya Miriam, mshtakiwa mwingine ni mfanyabiashara Revocatus Muyela.

Katika kesi ya msingi, washtakiwa hao wanadaiwa Mei 25, 2016 walimuua kwa makusudi dada wa marehemu bilionea Erasto Msuya, Aneth Msuya.

Related Post