Entertainment Social

Mzee aanika ugonjwa unamsumbua

Imeandikwa na Admin

Mchekeshaji maarufu Bongo, Amri Athumani alimaarufu kama ‘#MzeeMajuto’ amefunguka na kuweka wazi ugonjwa ambao unamsumbua kwa sasa kuwa ni tezi dume na kudai kuwa atafurahi sana endapo atafanyiwa upasuaji na kuondolewa maradhi hayo.

Mzee #Majuto ambaye kwa sasa yupo jijini Dar es Salaam na tayari ameanza hatua za awali kuhakikisha kuwa anafanyiwa upasuaji kuondolewa tezi dume amesema kuwa kutokana na umri wake hashangazwi yeye kupata ugonjwa huo na kudai ni ugonjwa tu kama yalivyo magonjwa mengine.

Related Post