Entertainment

Pretty Kind Aomba radhi kwa picha za nusu uchi

Imeandikwa na Admin

Msanii Suzan Michael maarufu kama Pretty Kind amefunguka na kuomba radhi kwa Serikali na Watanzania kwa ujumla kutokana na vitendo vyake vya kupiga na kuweka picha mitandaoni za nusu uchi.

Akiongea leo baada ya kufungiwa na serikali kujihusisha kufanya kazi zozote za sanaa kwa miezi sita, Pretty Kind amesema kuwa amejifunza na kugundua kuwa alikuwa anafanya makosa hivyo sasa hataweza kurudi tena kufanya mambo hayo. “Naomba niombe radhi kwa Watanzania wote kwa hiki nilichokifanya natambua nimefanya kosa naomba msamaha aweze kunisamehe, pia naomba msamaha kwa mashabiki zangu kwa hiki kilichotokea nimejifunza hivyo nitakuwa Pretty Kind mwingine mpya na kufanya yale yanayotakiwa katika jamii” alisema

Related Post