Entertainment Social

Ray C atuma ombi kwa rais kuhusu mwanawake kuolewa

Imeandikwa na Admin

 

Msanii wa muziki Bongo, #RayC ametoa ombi kwa Rais Dkt. John Magufuli kuhusu wanawake kuolewa.

Muimbaji huyo amependekeza kuwa kusiwepo na mahusiano kati ya mwanamke na mwanaume hadi ndoa ili wanawake wengi waweze kuolewa. Kupitia Instagram yake ameandika;

Mzee mi na shida Moja! hawa wanaume hapa nchini wanajifanya wajuaji Sana! Ombi langu la mwaka huu kwako ni hili!Naomba upitishe sheria kama ya Sultan Qaboos wa Oman! Hakuna mahusiano ya Kimapenzi kati ya mwanamke na mwanaume mpaka wafunge ndoa!

Na yeyote atakaekutwa na mwanamke iwe hotelini! Guest house bila Cheti cha ndoa wapelekwe wote segerea!Nadhani itasaidia sana wanawake wengi kuolewa badala ya kuwa manungaembe! Utakuwa umewanyoosha kisawasawa hawa Wanaume zetu Tutaheshimiana!
July mwaka jana Ray C alikaririwa na kipindi cha FNL cha EATV akisema hayupo katika mahusiano na mtu yeyote kwani ameshapoteza muda katika mambo hayo hivyo hawezi kumpatia mtu nafasi hiyo tena kwani akili yake kwa sasa ameielekeza kwenye kazi.

 

Related Post