Entertainment Social

Huu ndio ukweri wa mahusiano ya Diamond na Baba yake

Imeandikwa na Admin

Baada ya tetesi za muda mrefu kuzagaa kuwa Msanii wa Muziki nchini Tanzania, #DiamondPlatnumz kuwa hana mahusiano mazuri na baba yake mzazi, Hatimaye Diamond ameweka wazi ukweli wote kwa kukanusha taarifa hizo.

Diamond amesema kuna watu wenye hira ndio wanaokuza mambo lakini yeye huwa anawasiliana naye na huwa anamsaidia pale anapokuwa na kitu.

Ingawaje Diamond amekiri wazi kwamba hana mazoea naye kama ilivyo kwa mama yake mzazi lakini hakuna bifu kama baadhi ya watu wanavyokuza mambo.

Kwa upande mwingine, Diamond amewakanya baadhi ya watu ambao wanampeleka baba yake hadi kwenye geti lake na kumpiga picha ili kuupotosha umma kuwa amemfungia geti baba yake, waache hiyo tabia kwa sababu inaathiri hadi familia nyingine.

Related Post