Entertainment Social

Gigy Money afunguka kuachana na mambo ya kitoto

Imeandikwa na Admin

MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Gift Stanford ‘#GigyMoney’ amefunguka kuwa kwa sasa ameachana na mambo ya kitoto ili kuwa mama bora kwa mwanaye anayetarajia kumpata.

Akizungumza nasi, Gigy alisema kutokana na kwamba anatarajia kupata mtoto hivi karibuni, amejikuta akiachana kabisa na mambo ya kitoto aliyokuwa nayo kabla ya ujauzito na sasa anafikiria mambo ya kiutu uzima zaidi.

“Nimekua kwa kweli, unajua huu ujauzito umenipa funzo la maisha na sasa naenda kuwa mama hivyo ili niwe mama bora lazima nibadilike kwa kila kitu siyo kuendelea na yale maisha ya kitoto ya kujiachia kihasarahasara,” alisema Gigy.

Related Post