Kwetu Bongo

Online Magazine

TFF YAITENGA YANGA SC ISHU YA KAKOLANYA

SHIRIKISHO la Soka Tanzania, limeitaka Yanga kutoa uamuzi juu la hatma ya aliyekuwa kipa wa timu hiyo Beno Kakolanya na ilipewa siku nne kutoa jibu.

Hii ni baada ya mchezaji huyo kupeleka malalamiko yake kwa TFF na lengo likiwa ni kuvuinja mkataba baada ya kuwa na mvutano kwa muda mrefu.

Kakolanya kupitia mwanasheria wake walipeleka malalamiko hayo kwa TFF na baada ya kuyapitia walitoa amri kuwa Yanga inatakiwa kutoa uamuzi juu ya hatma ya mchezaji huyo.

Akizungumza na Championi Jumatano, Meneja wa kipa huyu, Seleman Haroub alisema kuwa wanasubiri majibu baada ya TFF kuiamuru Yanga kutoa majibu kuhusiana na mchezaji huyo.

“Malalamiko yetu yalifika TFF wameyafanyia kazi kwa sehemu yao na waliipa ya muda kuanzia Jumatatu mpaka Alhamisi kutoa uamuzi juu ya Beno kama wanamuachia au laa.

“Hivyo kwa sasa tunasubiri kuona Yanga wameijibu nini TFF ndiyo tuweze kujua hatma yake na mustakabali wa mchezaji wetu,”alisema Seleman.

Championi lilizungumza na Ofisa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo alisema: “Suala lipo kwenye kamati wakimaliza wao ndiyo wataniletea kwa sasa siwezi kusema lolote.

HUZUNI KWA MONDI, FURAHA KWA ZARI
UBELGIJI: SAMATTA ATWAA TUZO YA MCHEZAJI BORA
Recommended
x