Kakobe: Ukimgusa mmoja, umetugusa wote

0
51

Dar es Salaam. Askofu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zachary Kakobe amesema katika zama hizi ukimshambulia kiongozi mmoja wa dini ni sawa na kuwashambulia wote.

Akizungumza leo Jumapili Mei 12 katika Kanisa la Ufufuo na Uzima lililopo Ubungo jijini Dar es Salaam linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima, Kakobe amesema kitendo cha kumgusa mmoja ni sawa na kuwasha moto.

Kakobe amesema hayo kabla ya kuanza mahubiri katika ibada ya Jumapili ndani ya kanisa hilo.

“Nyani akiwa mzee ujue amekwepa mishale mingi ila kwake hakuna mishale mipya,” amesema Kakobe na kuongeza, “Yote ilikuja na kudondoka na kumuachia funzo kuwa inakuja na ikifika mbele yao inatawanyika kwa njia saba.”

“Nianze kwa kusema Askofu Gwajima nimemthibitisha kuwa ni mtumishi wa Mungu, wewe uliyepo hapa usitange tange, usitafute kuja kwangu wala kwa yeyote hapa uko mahali salama.”

“Wengi hawafahamu mambo hayo yalianzia wapi hivyo niko hapa kwa ajili ya kuwaambia na niwathibitishie tu kuwa sisi tumepewa mamlaka ya kuponda kila kitu,” amesema.

Wezi Waiba vito vya dhahabu jumba la Mengi
Mtanzania aripotiwa kufa maji Marekani