Kwetu Bongo

Online Magazine

NANDY APATA AJALI, MENEJA WAKE AFUNGUKA

BASI aina ya Coaster lililokua kwenye msafara wa kuelekea Nandy Festival Sumbawanga limepinduka Mikumi usiku wa kuamkia leo. Msafara huo ulikuwa na Wasanii Juma Nature, Whozu, Stamina,Nandy,Barnaba, Roma, Billnass, Ice Boy na Willy Paul.

Maneja wa Nandy amesema Basi lililopata ajali kwenye msafara kuelekea Nandy Festival Sumbawanga lilikua limebeba Wapiga Band na Dancers na sio Wasanii, mpaka sasa Majeruhi wako Hospitalini Mikumi, hakuna kifo na safari inatarajiwa kuendelea asubuhi ya leo.

Ubingwa wa Ulaya wampa ulaji Klopp
HUZUNI KWA MONDI, FURAHA KWA ZARI
Recommended
x