Kwetu Bongo

Online Magazine

Ubingwa wa Ulaya wampa ulaji Klopp

WAMILIKI wa Liverpool wako mbioni kutaka kumuongezea mkataba kocha wa timu hiyo, Jurgen Klopp baada ya klabu hiyo kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya mwishoni mwa wiki iliyopita.

Mashabiki 750,000 walimkaribisha Klopp ambaye mkataba wake wa sasa unamalizika mwaka 2022 na wachezaji wake juzi walikaribishwa nyumbani baada ya kushinda 2-0 dhidi ya Tottenham katika fainali iliyofanyika Madrid, Hispania.

Wamiliki wa klabu hiyo, ambao ni Fenway Sports Group wanataka kuingia mkataba wa muda mrefu na kocha huyo mwenye umri wa miaka 51, raia wa Ujerumani.

“Jurgen ni kocha mzuri na ni muhimu katika klabu hii,” alisema mwenyekiti wa klabu hiyo, Tom Werner. “Wakati wachezaji wakimrusha hewani Jurgen baada ya ushindi wetu, walijua kuwa mashabiki wote wa Liverpool wanampenda na kumkubali kabisa.”

Hilo ni taji lake la kwanza kubwa tangu Klopp kuwasili Anfield mwaka 2015 na kocha huyo alisema amefurahishwa na mapokezi waliyopewa.

“Sijui hasa kuna watu wangapi wanaishi Liverpool, lakini nafikiri kuna nafasi kubwa kwa mashabiki wa klabu nyingine.” Liverpool, ambayo msimu uliopita ilifungwa katika fainali na Real Madrid, ilimaliza na poiti 97 katika msimu huu wa Ligi Kuu na ilifungwa mara moja tu msimu mzima, lakini ilimaliza ya pili nyuma ya Manchester City.

Utajiri wa Jay-Z umetokana na nini?
NANDY APATA AJALI, MENEJA WAKE AFUNGUKA
Recommended
BASI aina ya Coaster lililokua kwenye msafara wa kuelekea Nandy…
x