• Loading stock data...

Kwetu Bongo

Online Magazine

BAJETI YA SERIKALI 2019/2020 YAWASILISHWA BUNGENI

SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesema pato la wastani la kila Mtanzania lilifikia Sh2.4 milioni mwishoni mwa mwaka jana kutoka Sh2.3 milioni mwaka 2017.

Hayo yameelezwa leo Alhamisi, Juni 13, 2019 na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango,  wakati akiwasilisha bungeni jijini Dodoma taarifa ya hali ya uchumi wa taifa katika mwaka 2018 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2019/2020.

Amesema ongezeko hilo ni sawa na wastani wa asilimia 5.6 na takwimu hizo, ongezeko hilo ni sawa na Sh100,000 kwa kila Mtanzania.

Alitaja pia kwamba kiasi cha pato la wastani kwa kila mtu mwaka 2018 ni sawa na Dola 1,090 za Marekani ikilinganishwa na Dola 1,044 za Marekani mwaka 2017  ambalo ni  ongezeko la asilimia 4.4.

“Hadi Aprili 2019, amana katika benki za biashara ziliongezeka na kufikia Sh 21.3 trilioni kutoka Sh20.2 trilioni katika kipindi kama hicho mwaka 2018,” alisema.

TOZO NA MUDA WA LESENI ZA UDEREVA WAONGEZWA
Putin backs Moldova’s new government amid political turmoil

Recommended
Russian President Vladimir Putin has strongly backed Moldova’s new coalition…
Please wait...

Subscribe to our newsletter

Want to be notified when our article is published? Enter your email address and name below to be the first to know.