Isabel dos Santos: Mwanamke tajiri zaidi Afrika ‘aliipora Angola’

0
82

Isabel dos Santos

Hati zilizovuja zinaonyesha jinsi mwanamke tajiri barani Afrika alivyopata utajiri wake kupitia unyonyaji kwa nchi yake na ufisadi.

Isabel dos Santos alipata mikataba ya faida kubwa inayojumuisha ardhi, mafuta, almasi na simu wakati baba yake alipokuwa rais wa Angola, nchi iliyoko kusini mwa Afrika yenye utajiri wa maliasili.

Hati hizo zinaonyesha jinsi yeye na mumewe walivyoruhusiwa kununua mali za serikali katika safu ya mikataba mibaya

Bi Dos Santos anasema madai dhidi yake ni ya uwongo na kwamba kuna uwindaji wa kisiasa unaofanywa na serikali ya Angola dhidi yake.

Binti huyo ambaye ni wa rais wa zamani nchini humo ameifanya Uingereza kuwa nyumbani kwake na anamiliki mali ghali katikati mwa London.

 • Mwanamke tajiri zaidi Afrika kuwania urais Angola
 • Orodha mpya ya mabilionea 20 wa Afrika yatangazwa

Tayari yuko chini ya uchunguzi wa jinai nchini Angola kwa ufisadi na mali zake zimezuiliwa. BBC Panorama imepewa idhini juu ya ufikiaji wa hati zaidi ya 700,000 zilizovuja juu ya ufalme wa biashara wa bilionea huyo mwanamke barani Afrika.

Mpaka kufikia sasa, Isabel amechunguzwa na mashirika ya habari 37 ikiwa ni pamoja na gazeti la The Guardian na gazeti la Exresso la Ureno.

Asilimia 30 ya raia wa Angola wanaishi kwa umaskini chini ya dola mbili kwa siku
Image captionAsilimia 30 ya raia wa Angola wanaishi kwa umaskini chini ya dola mbili kwa siku

Andrew Feinstein, mkuu wa kituo cha ufisadi, anasema nyaraka zinaonyesha jinsi Bi Dos Santos alivyoinyanyasa nchi yake kwa kuwadhulumu watu wa kawaida wa Angola.

“Kila wakati amekuwa akionekana kwenye jarida moja la glossy na mahali pengine ulimwenguni, kila wakati anapofanya sherehe za kukata na shoka huko kusini mwa Ufaransa, anapofanya hivyo ni sawa na

ICIJ imezitaja stakabadhi hizo kama Luanda Leaks.

Uhusiano wa mafuta

Moja ya biashara yenye utata iliendeshwa kutoka London kupitia kampuni tanzu ya Angola nchini Uingereza Sonangol.

Bi Dos Santos ilikuwa akisimamaia kampuni ya Sonangol mwaka 2016, ambapo alipata ulizi wa rais ambaye ni baba yake Jose Eduardo dos Santos, aliyeiongoza nchi kwa miaka 38.

Lakini alipostaafu kama rai s mwezi Septemba mwaka 2017 alikabiliwa na hatari ya kupoteza wadhifa wake, japo aliyemrithi Bw. Jose Eduardo dos Santos alitoka chama chake.

Bi Dos Santos alifutwa miezi miwili baadae.

Raia wengi wa Angola wameshangazwa na hatua ya rais Joao Lourenço ilivyolenga maslahi ya kibiashara ya familia ya mtangulizi wake.

Hati zilizovuja zinaonyesha kuwa wakati anaondoka Sonangol, Bi Dos Santos aliidhinisha $58m ya malipo tata kwa kampuni ya ushauri huko Dubai inayoitwa Matter Business Solutions.

Matter Business Solutions invoice
Image captionHizi ni baadhi ya ankara za malipo Isabel dos Santos alizotia saini wiki iliyopita akiwa na kampuni ya Sonangol

Anasema hana nia ya kifedha kwa jambo lolote, lakini nyaraka zilizovuja zinaonyesha zilisimamiwa na meneja wake wa biashara inayomilikiwa na rafiki.

BBC Panorama inaarifu kuwa Bi Isabel alituma stakabadhi za kudai malipo zaidi ya 50 kwa Sonangol huko London siku ambayo alifukuzwa.

Bi Dos Santos anaonekana kupitisha malipo kwa kampuni ya rafiki yake baada ya kufutwa kazi.

Ingawa kazi fulani ya ushauri ilifanywa na kampuni ya Matter, kuna maelezo kidogo sana juu ya stakabadhi za kuhalalisha bili kubwa kama hizo.

Moja inadai euro 472,196 kwa gharama zisizojulikana, nyingine dola za 928,517 kwa huduma za kisheria ambazo hazijajulikana.

Malipo yenye utata

Mchezo ulikuwa ukichezeshwa kwa namna hii, malipo mbili tofauti na – kila moja inadai euro 676,339.97- kwa kazi ile ile, kwa tarehe hiyo hiyo na Bi Dos Santos akawa akisaini zote.

Mawakili wa Matter Business Solutions wanasema kampuni hiyo ilibuniwa kusaidia kuleta mabadiliko katika sekta ya mafuta na kwamba malipo hayo yalikuwa ya kazi ambayo ilikuwa imefanywa na kampuni zingine tanzu ilizokuwa imeipatia kazi.

“Kuhusu malipo yaliyohusiana ni jambo la kawaida kwa makampuni kuongeza gharama katika malipo mengine kwa ujumla. Hii inatokana na gharama inayohusiana na kazi za kuweka pamoja mchakato mzima wa kujiandaa kikazi… Matter inaweza kuwasilisha stakabadhi za kuthibitisha hilo kukadiria gharama zote ilizolipa.”

Mawakili wa Bi. Dos Santos wamesema hatua yake kuhusiana na malipo ya kampuni ya Matter ilikuwa halali na kwamba hakuidhinisha malipo yoyote baada ya kufutwa kazi Sonangol.

Walisema: “Malipo yote yaliyohusiana na huduma ilizotoa ilikuwa makubaliano kati ya washirika wawili wa kibiashara, ambayo yalijumuishwa katika mkataba ambao ulifikiwa chini ya ufahamu wa wakurugenzi wa bodi ya usimamizi ya Sonangol.”

Nyaraka za benki zilizosainiwa na Isabel dos Santos zinaonesha alihamisha karibu $58m kutoka kampuni ya mafuta ya serikali ya Angola
Image captionNyaraka za benki zilizosainiwa na Isabel dos Santos zinaonesha alihamisha karibu $58m kutoka kampuni ya mafuta ya serikali ya Angola

ICIJ na Panorama pia imepata maelezo kuhusu biasha iliyomfanya Bi Dos Santos kuwa tajiri.

Sehemu kubwa ya mali yake ilikuwa kupitia umiliki wa hisa katika kampuni ya kawi ya Galp ya Ureno, ambayo ilikuwa moja ya makampuni yaliyonunua mafuta kwa kampuni ya mafuta ya Sonangol mwaka 2006.

Stakabadhi zinaonesha kuwa alihitaji kulipa 15% ya bei halisi mwanzoni na kukamilisha fedha zilizosalia ya €63m ($70m) ambayo ilibadilishwa kuwa mkopo wa riba ya chini kutoka Sonangol.

Chini ya mkopo huo wenye mashariti hafifu na ya kuvutia, deni lake kwa watu wa Angola halikuhitaji kulipwa kwa miaka 11.

Umiliki wake katika kampuni ya Galp sasa ni wa thamani ya zaidi ya €750m.

Kampuni ya Bi Dos Santos ilijitolea kulipa deni la Sonangol mwaka 2017.

Ofa ya kulipa deni hili ingelikuwa imekataliwa kwa sababu haikujumuisha riba ya €9m iliyokuwa inadaiwa.

Lakini Bi Dos Santos alikuwa msimamizi wa Sonangol wakati huo na alipokea fedha hizo kama malipo kamili ya deni alililokuwa akidaiwa.

Alifutwa kazi miaka sita baadae na malipo hayo yalirudishwa na usimamizi mpya wa Sonangol.

Bi Dos Santos anasema wazo la kuwekeza katika kampuni ya Galp lilikuwa lake na kwamba kampuni ya Sonangol pia ilifaidika na uwekezaji huo.

“Hakuna makosa yoyote ylaiyotokana na biashara hiyo. Uwekezaji huu ni uwekezaji ambao katika historia umefaidi kampuni ya kitaifda ya mafuta na kandarasi zote zilizoandikwa zilizingatia sheria, kwa hiyo hakuna makosa yaliyofanyiika.”

Mawakili wake wanasema ofa ya kulipa deni mwaka 2017 ilijumuisha deni ambalo lililokuwa linadaiwa na Sonangol.

Uhusiano wa almasi

Tawira katika sekta ya almasi noi sawa na ile ya mafuta .

Bi Dos Santos na mume wake, Sindika Dokolo, walitia saini mkataba ulioegemea upande mmoja mwaka 2012 na kampuni ya kitaifa ya almasi ya Angola,Sodiam.

Walitakiwa kuwa washirika wa kibiashara watakaonufaika nusu kwa nusu katika mkataba wa kibiashara na kampuni ya vito vya thamani ya Uswizi ya De Grisogono.

Isabel dos Santos na Sindika Dokolo wakiwa katika hafla ya de Grisogono wakati wa ukumbusho wa 69 ya tamasha la filamu la Cannes katika hoteli ya du Cap-Eden-Roc Mei 17, 2016 mjini Cap d'Antibes,Ufaransa
Image captionIsabel dos Santos na mume wake Sindika Dokolo mara nyingi huonekana katia matamasha ya filamu wakijumuika na waigizzaji wa kimataifa

Lakini uwekezaji huo ulifadhiliwa na kampuni ya serikali. Stakabadhi zinaonesha kuwa miezi 18 baada ya uwekezaji huo, Sodiam ilikuwa imelipa $79m katika ushirikiano huo, huku Bw. Dokolo akiwa amewekeza $4m pekee.

Sodiam pia ilimpatia €5m kwakufanikiwa kuleta biashara hiyo, hii inamaanaisha hakuhitaji kutumia fedha zake kulipia uwekezaji huo.

Bishara ya almasi ndio iliyowamaliza kabisa watu wa Angola.

Stakabadhi zilizofichuliwa zinaonesha jinsi kampuni ya Sodiam ilivyokopa fedha kutoka fedha kutoka kwa benki ya kibinafsi ambayo Bi Dos Santos alikuwa mwanahisa mkuu.

Sodiam italazimika kulipa riba ya 9% na mkopo wa ambao ulioidhinishwa na mamlaka ya rais, ili benki ya Bi Dos Santos isipate hasara.

Bravo da Rosa, afisa mkuu mtendaji mpya wa Sodiam, aliambia Panorama kuwa watu wa Angola hawakupata ha dola moja kutoka kwa uwekezaji huo: “Mwisho wa siku, tutakapomaliza kulipa deni hilo, Sodiam itakuwa imepoteza zaidi $200m.”

Rais wa zamani wa Angola pia alimpatia mume wa Bi Dos Santos haki ya kununua almasi ambayo haijasafishwa.

Isabel dos Santos akiwa amevalia rinda la Dolce & Gabbana wakati wa hafla Ambrosetti mjini Villa d'Este. Cernobbio, Italy
Image captionIsabel dos Santos

Isabel dos Santos ni nani?

 • Mwana mkuu wa aliyekuwa rais wa taifa hilo Jose Eduardo Dos Santos
 • Ni mke wa mfanyabiashara wa Congo Sindika Dokolo
 • Alihudumu katika shule ya upili ya wasichana ya mabweni nchini England.
 • Alisomea uhandisi wa umeme katika chuo kikuu cha Kings College mjini London.
 • Akiwa na miaka 24 alikuwa akimiliki hisa katika mgahawa wa Miami Beach uliopo mjini Luanda
 • Aliinuka na kuwa mwanamke tajiri zaidi barani Afrika
 • Alichaguliwa kuongoza shirika kuu la mafuta nchini Angola la Sonangol 2016 na kufutwa kazi 2017.
 • Ana hisa za asilimia sita katika mafuta ya Ureo na kampuni ya gesi ya galp ambayo ni thamani ya $830m
 • Anamiliki 42.5% ya benki ya Portugal ya Eurobic bank
 • Ana asilimia 25% ya hisa katika kampuni ya simu ya Unitelnchini Angola
 • Pia ana 42.5% ya hisa katika benki ya Angola kwa jina Banco BIC

Serikali ya Angola inasema kwamba almasi hizo ziliuzwa kwa bei isiojulikana na duru zimeambia panorama kwamba huenda takriban dola bilioni moja zilipotea.

Bi dos Santos aliambia BBC hakuweza kuendelea kwa kuwa hakuwa mwanahisa wa DeGrisogono.

Lakini stakhabadhi hizo zilizofichuliwa zimeonyesha kwamba alielezewa kuwa mmiliki wa hisa za De Grisogono na mshauri wake wa kifedha.

Bwana Dokolo aliwekeza baadaye. Mawakili wake wanasema kwamba aliwekeza takriban dola milioni 115 na kwamba ununuzi wa De Grisogono lilikuwa wazo lake.

Anasema kwamba kampuni yake ililipa kiwango zaidi ya kilichopokuwa sokoni kununua almasi.

Uhusiano wake na ardhi

Nakala zilizofichuliwa pia zilibaini jinsi bi santos alivyonunua ardhi kutoka kwa serikali mnamo mwezi Septemba 2017. Kwa mara nyengine alilazimika kulipa fedha kidogo.

Kampuni yake ilinunua kilomita moja ya ardhi ya ufukweni mwa bahari katika mji mkuu wa Luanda kupitia usaidizi wa amri ya babake aliyekuwa rais wakati huo.

Kandarasi hiyo inasema kwamba ardhi hiyoilikuwa na thamani ya dola milioni 96 , lakini kampuni yake ililipa asilimia tano ya makubaliano hayo ili kuwekeza zilizosalia katika kipande hicho.

Panaorama iliwachungza baadhi ya raia nchini Angola ambao walitimuliwa ili kutoa nafasi ya uwekezaji huo wa Futungo development.

Walihamishwa kutoka kutoka ufukwe wa bahari wa Luanda hadi eneo la ujenzi wa nyumba lililotengwa yapata kilomita 50 kutoka mji mkuu.

Teresa Vissapa alipoteza biashara yake kwa bi Dos santos na sasa anatatizika kuwalea watoto wake saba.

Alisema: Nitamuomba mungu kumfanya afikirie zaidi hali yetu. Pengine hata hajui laini tunateseka. Bi Dos Santos alikataa kutoa tamko kuhusu uwekezaji wa Futungo Development.

lakini haikuwa ardhi ya pekee iliokuwa ikihusisha bi Dos santos ambayo iliwawacha watu bila makao.

Mwanamke tajiri Afrika afunguliwa mashtaka ya ulaghai