Mwanamke tajiri Afrika afunguliwa mashtaka ya ulaghai

0
138

Isabel dos Santos: Angola yamfungulia mashtaka ya ulaghai mwanamke tajiri barani Afrika

Mwanamke tajiri zaidi Afrika Isabel dos Santos amefunguliwa mashtaka ya ulaghai baada ya kutuhumiwa kwa kulipora taifa hilo na waendesha mashtaka.

Mwanasheria mkuu Helder Pitta Groz alisema kwamba madai hayo yanahusiana na wakati alipokuwa mwenyekiti wa kampuni ya mafuta ya Sonangol.

Watu kadhaa pia wametuhumiwa pamoja na bi dos Santos.

Pia unaweza kusoma:

  • Benki ya Ulaya yakata uhusiano na mwanamke tajiri Afrika
  • Mali ya mwanamke tajiri zaidi Afrika yakamatwa
  • Mwanamke tajiri zaidi Afrika kuwania urais Angola

Bwana Pitta Groz alisema kwamba kibali cha kimataifa cha kuwakamata iwapo watakosa kujiwasilisha mbele ya mamlaka ya Angola.

“Isabel dos Santos anatuhumiwa kwa usimamizi na ufujaji wa fedha wakati alipokuwa mwenyekiti wa kampuni hiyo ya Sonangol hivyobasi amefungliwa mashtaka ya usimamizi mbaya wa ofisi , kutumia ushawishi wake na kughushi stakhabadhi miongoni mwa uhalifu mwengine wa kiuchumi”, bwana Pitta Gross aliambia mkutnao na wanahabari siku ya jumatano jioni.

Uchunguzi kuhusiana na usimamizi wake wa kipindi cha miezi 18 katika kampuni hiyo ya mafuta kuanzia mwezi Juni 2016 ulianzishwa baada ya mrithi wake Carlos Satumino kuelezea mamlaka kuhusu uhamishaji wa fedha usio wa kawaida .

Stakhabadhi zilivuja wwiki hii zikidai kwamba bi Dos Santos , mwana wa aliyekuwa rais wa taifa hilo Jose Eduardo dos Santos , alijipatia mali ya thamni ya dola bilibo 2.1 kwa kulipora taifa lake.

Amekana madai hayo.

Tutazidi kukupasha…

Isabel dos Santos: Mwanamke tajiri zaidi Afrika 'aliipora Angola'
Iranian oil tanker pursued by US says it is going to Turkey