Mlipuko wa kirusi cha Corona wazua hofu China

0
338

Virusi vipya vya Corona vimesambaa kutoka mji wa Wuhan nchini Uchina hadi sehemu zingine, pamoja na Marekani, Japan, Taiwan, Thailand na Korea Kusini.

Mamlaka imehamasisha watu wasisafiri nje na ndani ya mji wa Wuhan wakati ambapo idadi ya waliokufa imezidi 6. Imethibitishwa kwamba virusi hivyo vinaweza kusambazwa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine na maafisa wanaonya kuwa idadi hiyo inaweza kuongezeka zaidi wakati wa sherehe za mwaka mpya wa China ambapo huenda ukasambaa zaidi na kuwa changamoto kuuzuia na kuudhibiti.

Sampuli ya virusi vya ugonjwa vilivyochukuliwa kutoka kwa mgonjwa na kuchunguzwa katika maabara na maafisa wa serikali pamoja na wale wa shirika la afya duniani WHO zimethibitisha kwamba ugonjwa huo ni ule wa Coronavirus.

Idadi kuu ya visa vya ugonjwa huu nchini China imepatikana katika mji wa Wuhan

Virusi hivyo ni familia kubwa ya virusi sita na kirusi hicho kipya kitaongeza idadi hiyo kufikia saba ambapo ni maarufu kwa kusababisha maambukizi miongoni mwa binadamu.

Virusi hivyo vinaweza kusababisha homa , lakini pia vinaweza kusababisha ugonjwa mbaya wa Sars ambao uliwauwa watu 774 kati ya 8,098 walioambukizwa katika mlipuko ulioanza China 2002.

Uchanganuzi wa jeni za ugonjwa huo mpya unaonyesha kuhusishwa karibu na ugonjwa wa Sars zaidi ya ugonjwa wowote wa Coronovirus.

Mamlaka ya China imeripoti visa 139 vipya vya ugonjwa huo usiojulikana katika siku mbili, ikiwa ni mara ya kwanza kwa maambukizi hayo kuthibitishwa nchini humo nje ya mji wa Wuhan.

Visa vipya vilibainika katika miji ya Wuhan, Beijing na Shenzhen.

Korea Kusini pia iliripoti kisa chake cha kwanza kilichothibitishwa siku ya Jumatatu baada ya Thaialnd na Japan.

Jumla ya visa vilivyoripotiwa sasa vinapita 200 na watu watatu tayari wamefariki kutokana na virusi hivyo.

Maafisa wa Afya wamegundua ugonjwa huo, ambao kwa mara ya kwanza ulipatikana mjini Wuhan mwezi Disemba.

Wanasema umesababisha mlipuko wa homa ya mapafu lakini mengi kuuhusu haujulikani.

Wataalama nchini Uingereza waliambia BBC kwamba idadi ya watu walioambukizwa huenda ikawa kubwa zaidi ikilinganishwa na idadi iliotolewa na maafisa huku takwimu zikisema huenda imefikia watu 1,700.

China imeahidi kuongeza juhudi zake za kuchunguza wiki hii ya sherehe za kuadhimisha mwezi mpya ambapo mamilioni ya Wachina watasafiri kujiunga na familia zao.

Je ni nani aliyeambukizwa?

Mamlaka katika mji wa kati wa Wuhan nchini China inasema kwamba visa vipya 136 vimethibitishwa wikendi iliopita na mtu watatu katika mji huo akafariki kutokana na virusi hivyo.

Kwa jumla mji huo pekee umethibitisha karibia visa 200 vya ugonjwa wa Coronavirus.

Kufikia Jumapili jioni , maafisa wanasema kwamba takriban watu 170 mjini Wuhan walikuwa wanatibiwa hospitalini , ikiwemo watu tisa ambao walikuwa katika halli mahututi.

Maafisa wa afya katika wilaya ya Daxing mjini Beijing, walisema kwamba watu wawili waliosafiri kuelekea Wuhan walitibiwa ugonjwa wa homa ya mapafu unaohusisswa na virusi hivyo.

Mjini Shenzhen , maafisa walisema kwamba mtu mwenye umri wa miaka 66 alionyesha ishara ya virusi hivyo baada ya kuitembelea jamii yake huko Wuhan.

Virusi hivyo pia vimesambaa ugenini. Visa viwili vilithibitishwa nchini Thailand kimoja Japan – vyote vikuhusisha watu kutoka Wuhan ama wale waliotembelea mji huo.

Korea Kusini iliripoti kisa chake cha kwanza kilichothibitishwa kuhusu ugonjwa huo siku ya Jumatatu.

Kituo cha udhibiti wa magonjwa ya mapafu nchini Korea kilisema kwamba mwanamke mmoja wa China mwenye umri wa miaka 35 alikuwa akiugua mwili kuwa na joto na tatizo la kupumua alipowasili nchini humo baada ya kutoka Wuhan.

Alitengwa na kutibiwa katika hospitali moja , walisema.

Maafisa wanasemaje?

Tume ya kitaifa ya afya nchini China siku ya Jumapili ilisema kwamba virusi hivyo vinaweza kukingwa na kudhibitiwa , huku akionya kwamba uchunguzi wa karibu unahitajika kwa kuwa chanzo cha maambukizi hakijulikani.

Wamesema kwamba hakukuwepo na visa vya virusi hivyo kusambaa kutoka mtu mmoja hadi mwingine lakini na kwamba vimevuka mpaka na kuingilia spishi kutoka kwa wanyama walioambukizwa baharini na soko la wanyama mwitu katika mji wa Wuhan.

Shirika la Afya duniani linasema kwamba vyanzo vya wanyama vinadaiwa kuwa chanzo kikuu cha virusi hivyo na kwamba kulikuwa na visa vichache vya maambukizi ya binadamu hadi binadamu wanaposhikana.

”Huku visa vingi vikifichuliwa na uchanganuzi zaidi ukifanywa, tutapata picha nzuri kuhusu athari ya ugonjwa huo na maeneo ulioambukizwa”.

Ilisema kwamba ongezeko la idadi ya visa hivyo nchini China linatokana na kuongezeka kwa mipango ya vipimo na utafiti wa virusi hivyo miongoni mwa wagonjwa wanaougua magonjwa ya mapafu.

”Watu wanaweza kupunguza hatari ya kuambukizwa ugonjwa huo kwa kuchukua hatua kama vile kuzuia kushikana na wanyama, kupika vizuri nyama na mayai na kuzuia kushikana na mtu yeyote mwenye ishara za homa”, ilisema.

Coronavirus: Wachina washauriwa kuzingatia usafi

Picha ya mtu aliyefunga kitambaa cha kuziba pua na mdomo ”mask” ili kujizuia kupata virusi ni sehemu ya kinga dhidi ya maambuki ya ugonjwa.

Kitambaa hicho cha kuziba mdomo ambacho ni maarufu katika nchi nyingi duniani kwa ajili ya kujizuia maambukizi, sasa kinatumika sana China baada ya mlipuko wa virusi vya corona ambapo watu wamepewa ushauri wa kuejiepusha na mahali palipo na msongamano wa watu.

Wataalamu wa afya wameelezea namna ‘mask’ hizo zinavyoweza kufanya kazi ili kuzuia virusi.

Kuna baadhi ya ushahidi ambao unadhania kuwa mask hizo zinaweza kusaidia kuzuia maambukizi kati ya mtu na mtu.

Mask ilianza kutumika kwa mara ya kwanza katika hospitali mwishoni mwa karne ya 18, lakini zilikuwa hazitumiki katika sehemu za umma mpaka mlipuko wa mafua ulipotokea Uhispania mwaka 1919 na kuuwa watu zaidi ya milioni 50.

  • Mlipuko wa kirusi cha Corona wazua hofu China
  • Je ni ugonjwa gani huu unaosambaa kwa kasi China?

Dkt David Carrington, wa chuo kikuu cha St George, mjini London, aliiambia BBC kuwa “‘mask zinazotumika wakati wa operesheni au upasuaji huwa haziwezi kufanya kazi vizuri katika maeneo ya umma kuzuia watu kupata maambukizi ya virusi vya bakteria wa hewa ambao wanaambukiza, kwa sababu zina nafasi za wazi na zinaacha macho wazi.

Lakini zinaweza kupunguza maambukizi kwa kiasi fulani ya kuwakinga watu katika maambukizi ya mkono na mdomo.

Utafiti uliofanywa kutoka New south Wales ulipendekeza kuwa watu huwa wanashika nyuso zao mara 23 kwa saa.

Jonathan Ball, profesa wa ‘molecular virology’ katika chuo kikuu cha Nottingham, alisema kuwa : “Katika tafiti moja ambayo ilifanywa hospitalini, inaonyeshha kuwa mask ya sura huwa nzuri kwa kuzuia maambukizi kama ilivyobuniwa.

Wabunifu waliotengeneza mask hiyo waliitengeneza kwa namna ambayo inaweza kuzuia vimelea vya hewani.

Ingawa , ukiangalia ufanisi wake kwa ujumla katika msongamano wa watu, takwimu zinaonyesha utofauti mdogo – Vilevile si rahisi kwa mtu kukaa na mask kwa muda mrefu ,” Prof Ball aliongeza.

Dkt Connor Bamford, wa taasisi ya afya ya Wellcome-Wolfson, iliyopo chuo kikuu cha Queen Belfast, alisema kuwa “utekelezaji wa kuweka mazingira safi ndio hatua rahisi zaidi ambayo inaweza kufanya kazi kwa uhakika”.

“Kuziba mdomo wakati unapiga chafya, kunawa mikono, na kujizuia kuziba midomo kwa mikono kabla ya kunawa, kunaweza kupunguza hatari ya maambukizi kupata virusi”, alisema.

Watu wanapaswa kuzingatia:

  • Kuosha mikono mara kwa mara na maji yaliyochemshwa na sabuni
  • Kuepuka kushika macho na pua kadri uwezavyo
  • Kufanya mazoezi na kula chakula bora

Dkt Jake Dunning, mkuu wa masuala ya afya nchini Uingereza alisema kuwa: “Ingawa kuna watu ambao wanahisi kuvaa mask usoni kutasaidia watu kupata maambukizi, kuna ushahidi mdogo sana kuwa kitendea kazi hicho kinaweza kuwanufaisha watu wakiwa nje kwa sababu imebuniwa kwa ajili ya kufanya kazi kwenye huduma za afya.

Alisema pia mask hizo hazijavaliwa vizuri, kubadilishwa kila wakati kunaweza kuwa salama haa katika mazingira ya kazi.

“Utafiti unaonyesha kuwa mask hiyo ilivaliwa kwa muda mrefu huwa inapongeza nguvu ya ufanyaji kazi wake, alisema.

Watu wangezingatia zaidi kufanya mazingira yao kuwa safi, kama hilo suala la usafi wangelipa kipaumbele, alisema Dkt. Dunning.

Isabel dos Santos: Mfanyakazi wa benki apatikana amefariki mjini Lisbon
Android L Will Keep Your Secrets Safer