Utatuzi wa matatizo makuu sita ya DR Congo kwa miezi 12

0
94

Rais wa Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo Felix Tshisekedi akiinua katiba ya taifa hilo tarehe kama ya leo mwaka jana

Wakati Felix Tshisekedi alipotawazwa kuwa rais katika taifa la Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo takriban mwaka mmoja uliopita, wengi walipongeza na kusema kwamba ni hatua ya kihistoria – ukiwa uchaguzi wa kwanza wa amani ambapo rais aliyekuwa akiondoka alimkabili mamlaka mrithi wake.

Kwa miaka kadhaa taifa hilo , lenye utajiri mkubwa wa madini ikiwemo viungo vya betri za kutumia umeme lilikuwa limezongwa na mzozo na ufisadi.

Kama mgombea mkuu wa chama cha upinzani cha UDPS, bwana Tshisekedi alimshinda mgombea aliyekuwa akipigiwa upatu na mtangulizi wake Joseph Kabila katika uchaguzi huo wa mwezi Disemba 2018.

  • Usalama DRC: Je mwaka mmoja wa Tshisekedi umezaa matunda?
  • Je unafahamu Ugonjwa hatari zaidi ya Ebola DRC?
  • Mauaji ya ‘kulipiza kisasi’ Beni: Tunachokifahamu kufikia sasa

Lakini matokeo yake yalipingwa na mgombea mwengine wa upinzani Martin Fayulu ambaye alisema kwamba yeye ndiye aliyekuwa mshindi halali.

Haukuwa mwanzo mwema kwa kiongozi ambaye alikuwa na matumaini ya kuliunganisha taifa lililokuwa likikabiliwa na changamoto chungu nzima ikiwemo swala la ugonjwa wa Ebola , vita vya miaka kadhaa katika eneo la mashariki, ukosefu wa miundo msingi na uchumi uliozorota.

Je ameyashughulikia vipi maswala haya sita?

1.Mzozo uliopo eneo la mashariki

Wakati alipotawazwa kuwa rais , rais huyo aliahidi kujenga Congo ilio dhabiti kwa lengo la kuvutia maendeleo kupitia amani na usalama.

Bwana Tshisekedi amejaribu kuimarisha usalama lakini licha ya hilo raia wa kawaida bado wana hofu na kwamba hawahisi kuwepo kwa usalama zaidi ya ilivyokuwa miezi 12 iliopita.

Changamoto mojawapo ilikuwa kuendelea kwa ghasia mashariki mwa taifa hilo, ambapo makumi ya makundi yaliojihami yanafanya uharibifu.

Jeshi limefanikiwa kulirudisha nyuma kundi la wapiganaji wa ADF , kundi la waasi ambalo linatoka Uganda lakini sasa limepiga kambi katika jimbo la Beni nchini DR Congo.

Lakini 2019, wapiganaji hao waliimarisha mashambulizi yao ya kulipiza kisasi dhidi ya raia, na kuwaua zaidi ya watu 200 katika kipindi cha miezi mitatu.

“Wakati wa kampeni zangu za uchaguzi , nilipata fursa ya kutembelea ,maeneo haya na nilikumbwa na tatizo hili ambalo linaniumiza moyo sana” , bwana Tshisekedi aliambia BBC.

”Nilichukua jukumu wakati huo la kufanya kila kitu ili kuleta amani”.

Rais huyo aliliamuru jeshi kuweka kambi yake mjini Beni , mji ulioshamiri mashambulizi ya ADF. Baadhi ya wanajeshi walibadilishwa , na kuleta nguvu mpya katika vita dhidi ya wanamgambo hao.

Katika vita vyake dhidi ya kundi jingine, viongozi wawili muhimu wa waasi wa Kihutu nchini Rwanda FDLR waliuawa.

Lakini makundi mengine madogo yaliojihami bado yanaendeleza biashara yao katika jimbo hilo huku wengine wakihusishwa na biashara haramu ya madini.

Mashambulizi dhidi ya raia yanaendelea huku makundi ya waasi ambayo hujahami na mapanga yakitekeleza mashambulizi wakati wowote.

Jeshi wakati huohuo limekosolewa kwa jinsi linavyopigana dhidi ya wapiganaji hao.

2. Mlipuko wa Ebola

Wakati alipochukua madaraka , rais alikabiliwa na kuenea kwa virusi vya ebola , mashariki mwa taifa hilo.

Umekuwa mlipuko mbaya wa Ebola duniani , ambao shirika la afya duniani WHO liliutangaza kama janga la kiafya linalohitaji dharura.

Kavota Mugisha Robert, a healthcare worker who volunteered in the Ebola response, decontaminates his colleague after he entered the house of 85-year-old woman

ReutersDR Congo Ebola outbreak

since August 2018

  • 3,416infected
  • 2,237died
  • 1,136survived

Source: WHO

Kutoaminiana kati ya wenyeji na maafisa wa afya , kunakosababishwa na hadithi za kale mbali na ukosefu wa habari, pamoja na mashambulizi dhidi ya maafisa wanaokabiliana na ugonjwa huo kunaendelea kuathiri vita dhidi ya ugonjwa huo.

Chanjo mbili kwa sasa zinatumika katika eneo hilo ili kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huo.

Serikali ya bwana Tshisekedi imepata usaidizi chungu nzima kutoka kwa mashirika ya kigeni na inaonekana kwamba kiwango cha maambukizi kimepungua, lakini WHO linasema kwamba ni vigumu kuthibitisha hilo kwa kuwa kuna maeneo kadhaa ambayo ni vigumu kuyafikia kutokana na ukosefu wa usalama.

Lakini kujiuzulu kwa waziri wa afya Oly Ilunga mwaka uliopita kufuatia kutofautiana kuhusu jinsi walivyokuwa wakikabiliana na tatizo hilo, kulibaini kwamba sio kla mtu katika kundi hilo alikuwa na maono sawa kuhusu jinsi ya kukabiliana na virusi hivyo.

3.Mlipuko wa ugonjwa wa surua/Ukambi

Bwana Tshisekedi pia amelazimika kukabiliana na ugonjwa wa Surua. Virusi hivyo vinavyosambaa kwa kasi vimeambukiza zaidi ya watu 300,000 tangu kuanza kwa mwaka 2019, huku visa vikiripotiwa katika kila mkoa kati ya mikoa 26 ya taifa hilo.

Takriban watu 6,000 wamefariki – iki ni zaidi ya wale wa Ebola kutokana na mlipuko ambao kulingana na WHO ndio mlipuko mbaya zaidi kuwahi kutokea kote duniani.

Serikali ya bwana Tshisekedi inayoungwa mkono na WHO na mashirika mengine ya kimataifa imewapatia chanjo zaidi ya watoto milioni 18 walio chini ya umri wa miaka mitano nchini humo.

Lakini ukosefu wa fedha za kununua chanjo za kutosha mbali na barabara mbaya umezuia uwezo wa makundi ya afya kumfikia kila mtu.

Uharibifu uliofanywa na milipuko ya Ebola pamoja na surua ni ushahidi wa matatizo ya kimsingi yanayotokana na uongozi mbaya , badala ya kipindi ambacho Tshisekedi ameweza kuongoza.

Serikali yake imefanikiwa kupata usaidizi kutoka kwa mashirika ya kigeni lakini ataendelea kukabiliwa na changamoto chungu nzima katika kipindi chake cha uongozi kilichosalia.

4: Ujenzi wa taifa hilo

Muda tu alipochukua madaraka , rais alianza kile alichokiita siku 100 za mipango ya dharura. Akiwa na uwezo mchache tulianza kujenga shule, kurekebisha hospitali , barabara, madaraja na kuweka ferri ili kusaidia usafiri wa kuvuka mito, aliambia BBC.

Shirika la wanaharakati linalochunguza matumizi ya fedha za umma nchini DR Congo Congolese NGO Observatory of Public Spending lilikosoa jinsi mtindo wa zabuni ulivyokuwa ukitolewa.

Cha kuongeza ni kwamba ni miradi michache iliokamilika na hiyo inawakilisha kiwango kidogo cha miundo msingi inayohitajika na taifa hilo.

5.Kukabiliana na njaa

Kutokana na mapato ya mtu wa kawaida, DR Congo ni mojawapo ya mataifa yalio na umasikini mkubwa zaidi duniani licha ya kuwa na utajiri wa madini.

Raia wengi wa Congo huishi chini ya dola mbili kwa siku kulingana na benki kuu ya dunia takwimu hizo zimekuwa zikiimarika tangu mwanzo wa karne ,lakini taifa hilo lina hatua kubwa za kupiga.

Rais amesema kwamba anataka kukabiliana na umasikini na katika juhdi hizo ameongeza matumizi ya serikali.

Katika kipindi cha miezi 12 , bajeti ya serikali iliongezeka kutoka dola biloni sita hadi dola bilioni kumi na moja.

Hilo limezua mjadala mwengine wa jinsi ya kuhangisha fedha. Imani maarufu iliopo miongoni mwa maafisa wa serikali ni kwamba uhaba wa fedha unaweza kukabiliwa kwa kuzuia ufisadi serikalini.

Msemaji wa rais amesema kwamba mfumo wa haki unaendelea kufanya uchunguzi.

Ulipaji kodi katika maeneo mengine , ikiwemo katika majengo, umeongezeka ili kulipia matumizi. Lakini watu wengi wa wanasubiri kuona iwapo hali yao ya kiuchumi itaimarika.

6. Wasiwasi wa kisiasa

Licha ya kushinda urais , bwana Tshisekedi amelazimika kukabiliana na mgogoro uliokuwa ukimkabili mtangulizi wake Joseph Kabila ambaye anamiliki idadi kubwa ya wabunge bungeni.

Majadiliano kati ya vyama hivyo viwili yalichukua takriban miezi saba kabla ya makubaliano kuafikiwa kwa lengo la kubuni serikali.

Uhusiano kati ya vyama hivyo ulisababisha wasiwasi mkubwa katika kipindi cha mwaka mmoja huku wanasiasa wa pande zote mbili wakilumbana na mara nyengine kupigana.

Lakini inaonekana kuna juhudi za kuhakikisha kwamba mambo yanafanyika.

Tangu alipochukua mamlaka , rais Tshisekedi aliunda mazingira ya kisiasa ambayo ni tofauti na yale ya miaka iliopita ya rais Kabila.

Wafungwa wa kisiasa wameachiliwa huru huku wapinzani wa kisiasa waliokuwa wakiishi mafichoni wakirudi katika taifa hilo, ambapo wana majukumu bila kuhofia ukandamizaji wa aina yoyote.

Health star ratings Kellogg reveals the cereal